washiriki walipata nafasi ya kusikiliza, kuuliza maswali na kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu maisha na nafasi ya Mtume (s.a.w.w) katika kuongoza Umma wa Kiislamu.
Sirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa baraka za Mwenyezi Mungu (S.W.T), leo hii siku ya Alhamisi, tarehe 21 Agosti 2025, Hawzat ya Imam Zaynul Aabidin (a.s) iliandaa kikao maalum cha kielimu kilichohudhuriwa na wanafunzi wote wa madrasa hiyo.
🔹 Mada kuu ya kikao hiki ilikuwa: “Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Uchanganuzi wa Maisha Yake Matukufu”.
Katika kikao hiki, Sheikh Jaber Jamal aliwasilisha utafiti wake, akichambua nyanja mbalimbali za maisha ya Mtume (s.a.w.w), hususan kipindi cha mwisho cha uhai wake na mafunzo yanayopatikana kutokana na historia hiyo.
🔹 Muda wa kikao ulikuwa saa moja, na ndani yake washiriki walipata nafasi ya kusikiliza, kuuliza maswali na kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu maisha na nafasi ya Mtume (s.a.w.w) katika kuongoza Umma wa Kiislamu.
🔹 Washiriki wa kikao walikuwa ni wanafunzi wote wa madrasa, jambo lililoleta mazingira ya mshikamano, ushirikiano na kujengeana maarifa ya pamoja.
🔹 Mahali pa kikao kilikuwa ni ndani ya Ukumbi wa Shule ya Imam Zaynul Aabidin (a.s), ambapo uongozi wa madrasa uliandaa mazingira bora ya kielimu na kiroho kwa ajili ya kikao hiki.
Mwisho wa kikao, wanafunzi walieleza kufaidika kwao na elimu iliyotolewa, na walihimizwa kuendeleza tafakuri juu ya maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama kielelezo bora cha maadili, uongozi na ibada.
Your Comment